Alhamisi, 8 Juni 2017

NAIBU waziri wa habari,burudani na michezo wa serikali ya wanafunzi ROCOTASO , katika Chuo cha Royal Baraka Mathay o ametoa tamko juu ya michezo itakayo chezwa mei 9 mwaka huu.

Na  Dionesia Mwala

  

Akizungumza na  Mwanaroyal  chuoni hapo Urafiki  jijini Dar es salaam Mathayo alisema michezo hiyo itajumuisha Mpira wa  miguu, Rede, na  mpira  wa kikapu michezo ambayo itampa fulsa ya kila  mwanafunzi aweze kujijenga kiafya na  kiakili pia.

Aidha aliongeza kua mchezo huo utakua wa  kuwakalibisha wanafunzi wapya ambao ni  wageni  pamoja na  wenyeji  ambao watajenga timu ya kikosi cha Royal FC itayokua timu  ya chuo.

Pia alisema kwa mujibu wa  kocha wa  kikosi wa  timu hiyo Rajabu Mnakane ambaye ni  kiongozi wa  timu  hiyo  anatarajia kuona mchezo mzuri.

"Natoa  wito kwa wanafunzi wanaoweza kucheza michezo niliyoitaja wajitokeze kwa wingi  kujiandikisha pia siku ya ijumaa kwa wingi  katika kukamilisha mchezo wa  siku hiyo tuweze kupata timu  ya Chuo,alisema Mathayo.

Hata  hivyo   Naibu waziri huyo alisema kutokana na kusua sua kwa michezo katika upande wa wasichana wizara hiyo imeongeza  mchezo wa  rede ili kuwawezesha kucheza michezo ambayo itawajengea ukakamavu.

"Pia napenda niwambie wanafunzi wasiangalie kipaumbele  pia katika  michezo sio  katika masomo tu michezo ni  sehemu ya elimu," alisema Mathayo.

Kwa upande  wake msimamizi wa  timu ya rede Elizabeth  Joseph  alisema baadhi ya wasichana wameanza kujitokeza na  kusema kua mchezo huo  utawajenga kiafya na  kiakili kwa wanafunzi.

pia aliongeza kua mchezo wa  rede unaweza kuchezwa na  with hata  wa  3   hivyo endapo watu hawatojitokeza   kwa wingi unaweza kuchezwa na wachache kutokana na  mchezo huo  ulivyo

" wanafunzi wamejitoeza binafsi napenda rede nawasihii wanafunzi waje  kujiandikisha kwa wingi  ila  endapo hawatojitokeza navyojua mchezo wa rede hata  tukiwa watatu tunaweza kucheza,"alisema Joseph.

Aidha Joseph aliitaka serikali mpya  ya wanafunzi kuboresha michezo mbalimbali chuoni. hapo hususa katika upande wa  wasichana jambo ambalo limekua changamoto chuoni hapo  katika serikali zilizopita.

Nae mmoja wa  wanafunzi ambaye ni  wa  kitivo cha  uwaandishi wa  habari chuoni hapo Mwanahamis Mohamed  amewaasa wanafunzi kujitokeza kwa wingi  katika  mchezo huo ili kufurahi pamoja

Pia alisema fulsa  za michezo zimekua hazipatikani Mara kwa Mara katika vyuo  vingi  itachangia kujenga umoja  na  kusema kua wizara ya michezo imesikia kilio chao.

Mohammed  alisema katika mchezo huo atashiriki vyema kabisa ambaye  amejiandikisha katika mchezo huo  na  amejianda vyema katika mchezo wa rede.

" Nawashauri wasichana wenzangu wajitokeze kwa wingi  kwa sababu fulsa kama  hizi  hua hazijitokezi Mara nyingi na waziri amesikia kilio cha wanafunzi cha muda  mrefu," alisema Mohammed.

Mwanaroyal haikuishia apo ilizungumza na  mmoja ya wachezaji katika upande wa  miguu Johnson Johnson ambae ni mwanafunzi wa  wa  muhula wa mwisho ambaye aliipongeza wizara kwa kuliona jambo hilo.

Aisha Johnson aliwasihii wanafunzi wa  muhula mpya kujitokeza kwa wingi  katika mechi  hiyo ili kuwajengea kujuana na  kuweza kupata kikosi kimoja kwa ambacho kitakua kikiwakilisha Chuo katika michezo mbali mbali.

" Mi nawasihii wanafunzi waje kwa wingi  katika huu mchezo na  wachezaji wajitokeze tuweze kupata hamasa ya kucheza pambano ambalo tulikua tukisubiri kwa muda  mrefu",alisema Johnson.

Hata  hivyo  Johnson  aliishukuru  serikali  mpya kwa kuaanda michezo hiyo ambapo  utawafanya wanafunzi kua na  umoja na  kuweza   kushirikiana   katika mbalimbali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni