Alhamisi, 8 Juni 2017

Na Amos Nyanduku

 Raisi 16 wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Royal ROOCOTASO, Mustapha Mwakibete,  ametangaza na kuwaapisha mawaziri  wa serikali ya wanafunzi wa ROCOTASO  lenye jumla ya mawaziri 10 na manaibu waziri 10 katika  wizara 10 ambao wanaunda serikali hiyo.

Zoezi hilo zililofanyika katika ukumbi wa kamongo  mei 31 ambapo mawaziri  hao warikula kiapo cha uaminifu mbele ya Rais wa serikali hiyo na wanafunzi  wa chuo hicho.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa zoezi hilo Rais Mustapha alisema kwa sasa  kazi imeanza na kuwataka mawaziri hao kufanya kazi na kupeleka ripoti ya utekelezaji wa kila wizara kwa mwezi ili kutathimini utekelezaji wa wizara moja moja.

"Kwa sasa kila wizara itakuwa inaleta ripoti kwa kila mwezi kwenye ofisi ya Rais na kwa  pamoja tunatafakari na kuona wapi pamefanikiwa na wapi tumekwama kama serikali na  kutafuta njia nyingine ya kulitekeleza kwa pamoja"

Aidha Mwakibete aliwataka wanafunzi wa chuo hicho kufuta taratibi ma sheria za chuo  hicho ikiwemo suala la uvaaji vitamburisho pindi mwanafunzi anapokuwa maeneo ya chuo.

Mwakibete aliwataka mawaziri hao kutekeleza majukumu yao kulingana na katiba na sheria za  ROCOTASO ambapo alisema kwa sasa kila waziri atatakiwa kuwasirisha ripoti ya utekelezaji kwa  kila mwezi.

kwa upande wake mmoja wa mawaziri waliokula kiapo kuwa waziri wa elimu wa serikali  ROCOTASO, Amani Makala aliwataka wanafunzi wa chuo hicho kutoa ushirikiano ili  serikali iweze kutekeleza majukumu yake.

"Sisi ni wawakirishi wa wanafunzi ushirikiano wao na sisi ndio kitu cha msingi kitakacho  tufanya ukukamilisha yale serikali iliyo yapangilia kupitia ilani ya uchaguzi hasa kwa masuala mazima ya elimu," alisema makala

Aidha Makala aliwasisitiza wanafunzi wa chuo hicho kuitumia serikali hiyo katika kutatua migogoro baina ya  walimu na wanafunzi kwa kufanya hivyo  itaepusha migogoro  kati ya  mwanafunzi na mwalim ambayo hupelekea baadhi ya mwanafunzi kutofanya vizuri kwenye  somo husika.

"Kama mwanafunzi anatatizo na mwalim fulani anatakiwa kwanza afikishe kwenye wizara husika ili serikali iwe inajua kinachoendelea kwani hiyo ndio njia sahihi ya kupunguza incomplete na sup  zinazotokana na migogoro kati ya mwalim na mwanafunzi, " alisema Makala.

Makala alipongeza hatua ya rais wa ROCOTASO kumweka atika baraza la mawaziri na kuahidi atatekeleza ilani ya uchaguzi hasa katika wizara yake ambayo ndio mama katika ilani ya serikali iliyopo madarakani.

kwa upande wa wanafunzi wa chuo cha Royal walipongeza hatua hiyo ya Rais wa chuo hicho kuteua baraza la mawaziri na kulitaka kutekeleza majukumu yao ikiwemo pamoja na kuhakikisha ahadi zilizo ahidiwa zinatekelenzwa.

akizungumza na Mwanaroyal gazeti mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho, John Chusi,  alisema kwa sasa serikali  imeshakamilika hivyo rais kupitia baraza lake atekeleze ahadi zake na kushughurikia  na kuzitatua changamoto zinazowakabili wanafunzi wa chuo hicho.

"Kwa sasa serikali iko tayari kwa kazi hivyo Rais anatakiwa kutumia baraza lake vizuri ili kufanuki  na kutimiza yote aliyotwahidi wanafunzi hasa kwa sasa kuna changamoto nyingi zinazotukabili kama wanafunzi kupitia hili baraza atatimiza kwa sasa tumpe muda kwanza, " alisema Chusi.

Aidha chusi alitaja baadhi ya changamoto ambazo angependekeza serikali baraza la mawaziri lianze kuzitatua ikiwemo suala la ucheleweshwaji na upatikanaji vitamburisho, ikiwa pamoja na suala zima la serikali kusimamia
suala hilo.

Hata hivo mmoja wa wajambuzi wa masuala ya siasa wa chuo cha Royal Alfred pitter alitoa tasimini yake kwa baraza mpya ambalo liliteuliwa may 31 mwaka huu na kupongeza hatua hiyo ambayo alisema itaimalisha utekelezaji wa majukumu ya serikali.

"Nampongeza Rais Mustapha kwa kuteua baraza dogo na lenye mawazirri ambao wanaweza kukidhi mahitaji yawanafunzi na kuzitatua changamoto zinazowakabili wanafunzi wa chuo hicho, ? Alisema Pitter.

pitter alisema Rais wa serikali ya wanafunzi ROCOTASO anachangamoto kubwa ya kutekeleza ilani yake ya uchaguzi ambayo imeainisha mambo mengi hivyo hana budi kulitumia baraza hilo kikamilifu na pia kuwasimamia mawaziri wake ikiwa pamoja na kila waziri kujua majukum yake kikamlifu.

"Mawaziri wote lazima wayajue majukum yao na nini kinatakiwa kufanyika ili kumpunguzia mzigo Rais kwa kuanza kufatilia kila kitu hivyo lazima kila wizara kupitia mawaziri wake watekeleze majukum yao na kujua mipaka ya kuyatekeleza yote haya, " Alisema Pitter

Uchaguzi mkuu wa Ris na makam wa Rais wa serikali ya wanafunzi ROCOTASO ulifanyika mnamo Mei 12 mwaka huu ambapo wanafumzi wa chuo cha Royal waliwachagua w`awakirishi wao katika nafasi hizo na zoezi la kula kiapo kwa Rais na makam wa Rais likafuata siku 2 baadae.

Uchaguzi mkuu wa ROCOTASO hufanyika kila baada ya miezi 12 kama katiba ya serikali ya wanafunzi ROCOTASO ambayo ni moja ya hatua ya kidemokorasia katika chuo hicho.







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni